Jumanne, 15 Juni 2021

Historia ya Grand P

Grand P Msanii Mwenye Mvuto wa Aina Yake 

  • Thread starte

Jina la kuzaliwa: Moussa Sanguiana Kaba Mwaka wa kuzaliwa: 1990 Umri: Miaka 31(mwaka huu 2021)
Kuzaliwa: Sanguiana (Guinea) Raia: Guinea
Kipaji: Mwimbaji, muigizaji, mtu wa mitandao ya kijamii na mwanasiasa
Aina ya muziki: Hip hop Miaka ya kazi: Tangu 2019
suala la kiafya: Kuugua progeria, ugonjwa adimu wa maumbile unaojulikana na kuzeeka mapema
Historia zaidi na Emmanuel Kasomi

Maswali ya kujiuliza kuhusu Grand P
Grand P alizaliwa lini? -Mwanamuziki hodari wa Guinea alizaliwa mnamo 1990, ambayo inamaanisha kuwa ana umri wa miaka 31 kwa sasa. Haijulikani sana miaka ya mwimbaji mwenye talanta. Pia, yeye mara chache anashiriki habari ya familia yake.
Grand P alizaliwa na ugonjwa nadra wa maumbile uitwao progeria, ambao unasababisha kuzeeka mapema ulioanza wakati wa kuzaliwa. Hali hiyo hupunguza urefu wa mtu kuwa mita mbili na uzani fulani. Msanii hodari amekuwa akidhihakiwa na kudhihakiwa kwa muda mrefu kwa sababu ya muonekano wake. Walakini, bila kujali hali yake, mwanamuziki maarufu anaishi maisha kwa ukamilifu na hata ana rafiki wa kike mzuri ambaye ni mtu wa Ivory Coast.
Sehemu ya kufurahisha zaidi ya wasifu wa Grand P Guinea ni kazi yake ambayo imepambwa kwa kushangaza. Leo, yeye ni mwigizaji mashuhuri, mwimbaji na hivi karibuni, mwanasiasa aliyeonyesha kupendezwa na kiti kikubwa cha kisiasa cha Guinea - Urais.
Je! Aliundaje haya yote? Grand P alikua maarufu wakati wa onyesho ambalo liliandaliwa na moja ya sanamu zake kubwa Kerfalla Kante kwenye Ikulu ya Watu huko Conakry. Tangu wakati huo, msanii huyo mwenye talanta alizidisha umaarufu wake na anaalikwa mara kwa mara kwenye matamasha kadhaa na hupokea ofa nyingi za kuonekana.
Wakati fulani, Grand P kutoka Guinea aliruhusiwa kuwakilisha na kuunga mkono ujumbe wa Guinea huko Cairo kwa CHAN (Kombe la Mataifa ya Afrika). Utambuzi kama huo katika nchi yake ya asili umesababisha mwanamuziki huyo kupata umaarufu katika Afrika na ulimwengu wote.

Je! Unashangaa utajiri wa Grand P?
Kasomi nimekuletea humu  kila kitu. Kwa kweli, mwanamuziki ana utajiri mwingi akizingatia kazi yake ya muziki iliyofanikiwa na vile vile anapenda shughuli zingine. Yeye haoni aibu kujivunia utajiri wake mtandaoni, akithibitisha kuwa ikiwa mtu ataweka bidii anayotaka, wanaweza kushinda vizuizi vyovyote wanavyopata. Walakini, hakuna kipimo rasmi cha thamani yake hadi sasa katika uwanja wa umma. Kwa miaka mingi, Grand P amekuwa akipata umaarufu mkubwa zaidi ya mipaka ya Guinea. Hakuna shaka kwamba thamani yake ya utajiri inakua sana.
Pia nimekusogezea hili.
Muziki wa Grand P Je! Unajua muziki wangapi wa Grand P? Msanii huyo wa Guinea ana albamu moja na kolabo kadhaa na wasanii tofauti. Ni kama ifuatavyo.
Grand P ameshirikiana na Azaya na vile vile Mfalme Alasko katika nyimbo zingine. Kwa kweli, Grand P labda anatafuta kuunda nyimbo zaidi katika siku zijazo. Ni mburudishaji anayefanya kazi kwa bidii na ustadi mkubwa wa biashara ambao umemwona kuwa mmoja wa wasanii maarufu nchini Guinea.

Je! Grand p ameoa?
Labda mada yenye utata na kujadiliwa mitandaoni kuhusu Grand P ni uhusiano wake. Hivi sasa yuko kwenye uhusiano na mwanamitindo wa Mkubwa wa Ivory Coast Eudoxie Yao. Wanandoa hao, ambao hushughulikiwa mara kwa mara mitandaoni mnamo Agosti 2020 na walipanga kuoana mapema 2021. Kumekuwa na ukosoaji mkubwa, watu wakidai kuwa wawili hao wako pamoja tu kwa faida ya kifedha. Walakini, wote wamesisitiza kwamba uhusiano wao ni wa kweli na wenye nguvu na hawajali uvumi wa watu na maoni ya jamii. Eudoxie ameandika hata kwenye Instagram yake, ambayo ana mamilioni ya wafuasi kuunga mkono umoja wao.
Grand P ni moja ya haiba maarufu nchini Guinea. Na amegundua jinsi ya kuchukua faida ya umaarufu na kufanya hatua kubwa za kifedha ambazo zimemwona akiongezeka kwa bahati kubwa. Hakuna shaka kuwa ana talanta katika maeneo ambayo anafanya mazoezi, iwe ni kuimba, kuigiza au katika uwanja wa siasa.

Hiyo ilikuwa ni Historia yake Grand P iliyo letwa kwenu na kijana wenu Emmanuel Kasomi

Jumatano, 5 Mei 2021

CHAMBILECHO FIDEL CASTRO, "MHUKUMUNI MWL BASHIRU, HISTORIA ITAMWACHIA HURU."

CHAMBILECHO FIDEL CASTRO, "MHUKUMUNI MWL BASHIRU, HISTORIA ITAMWACHIA HURU."

Na Sabatho Nyamsenda 

Leo nimeamka nikitafakari kuhusu mwalimu wangu Dk. Bashiru Ally. Tafakuri imenipeleka mbali hadi mwaka 2011, nikiwa mwaka wa tatu wa shahada yangu ya kwanza pale UDSM. Nyakati hizo nilikuwa mwenyekiti wa chama cha wanafunzi kilichojulikana kama Sauti ya Vijana Tanzania (SAVITA), huku Mwalimu Bashiru akiwa ndiye mlezi wetu. Mwaka huo, nilishiriki kuhariri jarida la Kigoda cha Taaluma cha Mwl Nyerere lililokuwa na lengo la kuadhimisha miaka mitatu ya "Kigoda", chini ya Prof Issa Shivji. 

Mimi na mhariri mwenzangu tulikusanya makala kutoka kwa Wana-Kigoda zinazohusu ya tafakuri zao juu ya shughuli za kitaaluma na kimapambano zilizoongozwa na Kigoda. Mchangiaji mmoja hakutuma makala bali shairi. Shairi liliitwa, "Heko Nyingi Nawapeni, Kwa Kutimiza Ahadi." Mchangiaji huyo ni Dk Bashiru Ally, enzi hizo tukimwita "Mwalimu Bashiru." Na alilighani shairi hilo katika Tamasha la Kitaaluma la Mwalimu Nyerere mwezi Aprili 2011.

Mwezi Mei 2011 SAVITA iliandaa Kongamano la Kuadhimisha miaka 44 ya Azimio la Arusha. Mtoa mada alikuwa ni Prof Shivji, na mwongozaji ni Mwl Bashiru. Baada ya kongamano hilo nilistaafu uenyekiti wa SAVITA. Katika hotuba yangu ya kukabidhi uongozi, niliandika maneno haya, huku nikinukuu baadhi ya beti kutoka kwenye shairi la Dk Bashiru nililolitaja mwanzoni:
________________________
"Kwa walioishika vema, SAVITA iligeuka kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku. Matendo yao, mazungumzo yao, mavazi yao, matarajio yao, mitazamo yao na hata maamuzi juu ya nani awe rafiki ama adui vilijengeka katika misingi ya SAVITA  niliyokwishaitaja hapo awali. Lakini, ashakum si matusi. Tuna jamii ya ajabu. Katika zama hizi za utandawazi, kuishika misingi hiyo ni ‘uendawazimu’. Tuna jamii ambayo itakushangaa usipoiba, itakukujeli usiposema uongo na itakutukana ukijidai una moyo wa kujitolea. Mwalimu Bashiru Ally aliyaona hili, ndio maana akaghani:

"Vita mliyoasisi, ni vita ya ukombozi,
Kukomboa Almasi, na samaki wa Zambezi,
Vilevile kuziasi, sera za ‘utandawizi’,
Heko nyingi nawapeni, kwa kutimiza ahadi.

"Vita ikishakolea, mtaiwa magaidi,
Hongo msipopokea, mtaitwa wakaidi,
Ushindi ukiwadia, mtaitwa mashahidi,
Heko nyingi nawapeni, kwa kutimiza ahadi."
___________________________

Miaka 10 imepita tangu niitoe hotuba ile. Sikujua kuwa niliyokuwa nikiyasema ndiyo yatamkuta gwiji huyu wa mapambano. Na shairi la Dk Bashiru pia limetimiza miaka 10. Nafikiri wakati akiliandika na kulighani hakuwa amejua yatakayotokea leo. 

Kosa pekee alilofanya ni kuokoa mali za chama chake, ambapo hapo awali zilisemekana kuwa na thamani ya bilioni 60, ila baada ya uhakiki wa Kamati aliyoingoza ikagundulika kuwa zina thamani ya trilioni 1 (kwa mujibu wa vyombo vya habari). Mali za zaidi ya bilioni 940 zilikuwa zimeporwa na walafi, huku chama chake kikiwa kimewekwa mfukoni mwa mafisadi. Hao ndio wanaoongoza kumchafua leo hii. 

Mara baada ya kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM, ziara yake ya kwanza aliifanya katika ofisi za Mtandao wa Wakulima Wadogo Tanzania - MVIWATA. Haikuwa mara ya kwanza kufika hapo bali alikuwa ni rafiki wa MVIWATA kwa muda mrefu kabla ya kuteuliwa. Hiyo ilifungua mlango mpya wa mshikamano katika kupambana dhidi ya uporaji wa ardhi, mbegu za kifo za GMO, rasimu ya sera mpya ya kiporaji ya ardhi, nk. Vijiji vya Msowero (Kilosa), Lukonde na Mtego wa Simba (Morogoro Vijijini), Mchukwi (Kibiti), Amboni (Tanga), na kwingineko vinamkumbuka kwa jinsi alivyoungana nao kupambana na mtandao wa waporaji wa ardhi, waliokuwa wakichoma nyumba za wanavijiji, kuwapiga na kuwafungulia wanavijiji mashtaka ya kughushi na kuchoma mazao yao mashambani. Haya huwezi kuyasikia kwenye vyombo vya habari. Kwa wavujajasho hao waliporwa ardhi, Mwalimu Bashiru ni shujaa. Huko wanamwombea dua na kumtakia heri. Ni nani atakayesikia sauti zao?

Mwaka jana, nikizungumza na Fr. Privatus Karugendo, aliniambia kuwa alishangazwa sana alipofika nyumbani kwa Bashiru akiwa katibu mkuu wa CCM. "Nyumba iko tupu. Anaishi maisha very simple," Fr Karugendo alinambia, huku akifurahi kuwa cheo hakikum-badilisha Bashiru. Hata alipolazimika kuvaa suti katika dhifa za kitaifa, alivaa 'suti za Kaunda' na sio koti na tai. Lakini vyake ni viatu vya wazi (sandles), suruali na shati.  
 
Bashiru sio mtu wa vyeo na wala hakugombea cheo chochote. Aliteuliwa. Huyu ni mjamaa na wanamajumui wa Afrika. Samaki kwake majini, mjamaa kwake mapambanoni. Mwalimu wake, Nyerere, alipotoka Ikulu alirudi Butiama kushika jembe na kucheza bao na wanavijiji. 

Natumai Mwl Bashiru atakapomaliza kutumikia nafasi yake ya uteuzi ya sasa, atarudi chuoni kufundisha, kutafiti na kushiriki katika mapambano ya wavujajasho kudai haki zao. Natumai tutapanda wote basi kwenda Morogoro kwenye mikutano ya MVIWATA. Natumai tutapanda tena bodaboda kwenda vijijini kujifunza kwa wavujajasho. Natumai atatutungia na kutughania mashairi ya kimapinduzi. Natumai tutakusanya tena maandiko ya wanamapinduzi, kuyatafsiri na kuyachapisha.

Fidel Castro alipotiwa korokoroni kwa kupambana dhidi ya ujahili nchini Cuba, alisema, "Nihukumuni. Historia itaniachia huru." Naam, historia ya mapambano dhidi ya ufisadi na uporaji wa rasilimali za wavujajasho itamwachia Mwl Bashiru huru. Na historia hiyo haitaandikwa na walafi na mafedhuli aliopambana nao. Itaandikwa na wakulima wadogo, wamachinga na bodaboda.

Jumanne, 27 Aprili 2021

JIFUNZE KUMUACHA AENDE

JIFUNZE KUMUACHA AENDE

• Kamwe usihisi kama ulimwengu ndio unakaribia mwisho pale akupendae anapokuacha.

MUACHE AENDE !

• Kujaribu kumlazimisha mtu akupende ni sawa na kujaribu kumlazimisha Nguruwe kutambua usafi na uzuri. Usimlazimishe akupende, mwache mwenyewe akupende, kama hakupendi...

MWACHE AENDE !

• Wewe ni wa thamani mno kulilia penzi. Mtu ambae anakupenda kweli atakuheshimu na hataku 'treat' kama uchafu. Kama atakuchukulia wewe kama uchafu...

MUACHE AENDE !

• Usipoteze muda wako wa thamani kujaribu kumshawishi au kuomba mapenzi. Mtu mwingine pembeni anakupenda wewe kwa dhati, ila wewe uko busy mno kumuogesha nguruwe! Kwanini?

MUACHE AENDE !

• Usikasirike pale mtu wako anapompenda mwingine tofauti na wewe. Siku zote hua ni vigumu kumshawishi NYANI kwamba Asali ni tamu kuliko ndizi...

MUACHE AENDE !

• Mwanamke/mwanaume yeyote anaekuchukulia kirahisi siku zote atachukulia faida kwako, atakugeuza atakavyo kama chapati akijua hufurukuti, yeye sio Mungu wa kukufanya atakavyo...

MUACHE AENDE !

• Kuna watu hawatakupenda hata kama utajitoa kiasi gani kwao. Ni sawa tu. Kukukataa kwao haimaanishi kwamba una kitu kibaya, bali ni maana kwamba hawako kwa ajili yako. Usilazimishe duara kuwa pembe tatu...

MUACHE AENDE !

CHA KUJIFUNZA

• Hauwezi badilisha maoni mabaya ya watu juu yako, ila unaweza ukazuia maoni yao mabaya yasikubadilishe wewe kama wewe!

• Acha kichwa chako kiongoze moyo wako kukuondoa katika mahusiano sumu. Lengo la mahusiano sio kuleta mafadhaiko ila ni kuongeza furaha juu ya ile uliyokuwa nayo mwanzoni ulipokuwa haupo ktk mahusiano.

NI NGUMU SANA ILA KWA MUSTAKABALI WA FURAHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE ME NAKWAMBIA MUACHE AENDE MPE NA NAULI KABISA!

Kama ipo ipo tu...!

Tupo pamoja??

KINACHOMTESA MEYA JUMA RAIBU NI KAZI ZAKE

KINACHOMTESA MEYA JUMA RAIBU NI KAZI ZAKE

Anaandika Mwinjilisti Mathayo Chamshama

Trending news ya sasa katika siasa za kaskazini ni Juu ya kinachoitwa "Uchotwaji wa Milioni 150 za Benki ya KCBL" ambapo anatuhumiwa Mstahiki Meya wa Moshi Mhe Juma Raibu Juma, ambae ni mteja wa Benki hiyo wa muda mrefu hata kabla ya kuingia kwenye Siasa.

Mimi nimemfahamu Raibu akiwa hana "Uheshimiwa" wowote ule, alikuwa mfanyabiashara anaekuja kwa kasi sana katika Manispaa yetu, na nimeifatilia hii habari kwa undani nimembulia kung'amua mambo kadhaa yaliyonipa jibu ya Chanzo cha ili suala la uzushi na uongo lililopikwa kwa ustadi ila likakosa timing na angle nzuri, Hakika lingewekwa kwenye angle na timing sahihi lingeweza kumzima kisiasa Raibu kama ilivyokuwa imekusudiwa hasa kumwondoa kwenye cheo cha Umeya wa Manispaa.

Nimeongea na rafiki yangu wa KCBL amenidokeza kuwa Meya ni Mteja wao na hilo suala linalotumika sasa ni tukio la mwaka 2013 ambapo benki hiyo ilifanya makosa ikawaingizia wateja zaidi ya 30 wa (Fixed Deposit) Faida ya Riba ya kiwango kikubwa tofauti na mikataba yao hivyo Raibu wa miaka hiyo nae alikuwa mnufaika japo hakuwahi kuitoa ile fedha, Suala hilo liliisha kwa KCBL kutoa milioni 154 zilizozidi kwenye akaunti ya Mteja wao huyo na wengineo kwa viasi sahihi.Takukuru katika kuzipitia kesi hizo za wateja hao hawakumtaja hawakutoa taarifa ya kumshutumu Meya huyo kwa suala hilo ila kuna baadhi ya "Vigogo Ngazi ya Mkoa" maadui wa Mhe Raibu waliponasa kuwa nae ni mteja wakaamua kutengeneza hii tension mitandao kwa maslahi yao.

Tatizo kubwa linalofanya Meya huyu apitie haya ni kazi zake anazozifanya kwa wananchi wa manispaa hiyo hasa zile za sakata la kurejesha zaidi ya milioni 90 zilizokuwa zimeporwa na Saccos za Wahalifu fulani wenye nguvu ya pesa mkoani hapa, Sakata la kuwadhibiti wazabuni uchwara, Sakata la kudhibiti taasisi zisizowasilisha makato NSSF, urejeshaji wa mashamba,viwanja vya wanyonge na lile la kuvunja majengo yaliyojengwa kinyume cha sheria ya mipango miji. Hayo ndio yamemjengea maadui wakubwa wanaokesha na kuungana kuhakikisha anang'oka kwenye cheo hicho ambacho kimekuwa mwiba wa upigaji dili wa miaka yote.

Wosia wangu kwa Meya huyu either akomae kupigania wanyonge ili achukiwe au aungame kwa wapiga dili asalimike, kazi kwako Meya Juma Raib.

Mwinjilisti Chamshama

Jumatano, 21 Aprili 2021

Store Keeping

Store Keeping

By kasomi kasomi

After materials purchased have been received and checked, the next step in the process of material control is the storing of materials or store keeping.

‘Store keeping’ refers to the safe custody of all items of raw materials, supplies, finished parts, purchased parts etc., in the store-room for which the store-keeper acts as a trustee. It is said to be the process of receiving and distributing stores or supplies.

According to Alford and Beatty, “Store keeping is that aspect of material control concerned with the physical storage of goods.”

In the words of Wheldon, “Store keeping is the physical storage of materials carried into the store-room in a scientific and systematic manner with a view to (i) saving them from all kinds of damages and losses, and (ii) exercising overall control over their movement.”

In short, store keeping refers to the art of preserving raw materials, work-in-progress and finished parts in the stores in the best possible manner. Generally, in small concerns, no importance is given to stores department. But it should be remembered that material pilferage, deterioration of materials and careless handling of materials lead to reduced profits or even losses. As such, it is necessary to maintain a well-equipped stores department to ensure maximum efficiency. Spriegel and Lansburgh have rightly remarked— “Poor control of materials is frequently accompanied by poor store-room administration in a way that may easily throw out of balance any operation programmes which have been adopted.”

Objectives Of Store Keeping
An efficient system of store keeping has the following objects:

To ensure uninterrupted supply of materials and stores without delay to various production and service departments of the organization.
To prevent over-stocking and under-stocking of materials.
To check in all materials as to quality and quantity.
To minimize storage cost.
To ensure proper and continuous control over materials.
To ensure most effective utilization of available storage space and workers engaged in the process of store-keeping.
To protect materials from loss and wastage due to defective storage.
To identify and locate materials in the store-rooms without delay.
To protect and safeguard material items against pilferage, theft and fire etc.
To develop such a system so that fullest information about store items is available in the stores at every time.
Functions of Store Keeping
The principal functions of store-keeping to be performed by the Stores Department in an organization, are as follows:

Issuing purchase requisitions as and when material is required.
Receiving purchased stores from the Receiving Department and verifying that every lot of stores is supported by an indent, a purchase order and an inspection note.
Preparing ‘Goods Received Note’ in accordance with the different stores lots received.
Ensuring that all the Goods Received Notes are regularly posted to the Bin Card.
Placing and arranging stores received at proper and appropriate places and adhering to the golden principle of store keeping i.e., ‘A place for everything in its place. ‘
Minimizing the storage, handling and maintaining costs by preserving and handling the materials in the most economical and efficient manner.
Issuing stores to various departments of the business and ensuring that all issues are properly authenticated and accounted for.
Ensuring the adherence to the proper issuing procedure and system followed in the organization.
Taking a periodical review of inventory by initiating various inventory control systems viz., perpetual inventory control system and ABC system of inventory control.
Disclosing fullest and up-to-date information about the availability of stores whenever required, by maintaining proper stores records with the help of Bin Cards and Stores Ledger.
Ensuring proper safety of materials against theft, pilferage and fire, etc.
Supervising and co-ordinating the duties of different types of staff working under the headship of the store-keeper.
Preventing entry of unauthorized persons in the stores.
Maintaining proper stock-levels fixed in respect of every item of stores and replenishing them as and when necessary.
Store keeper and his duties
As we know that in a manufacturing concern, stores or materials represent an equivalent amount of cash. As such there should be a proper system of store-keeping which will ensure the safe custody of materials, easy location of the various items of stores, economic usage of storage space, regular and efficient flow of materials, maintenance of reliable stores records and an efficient assessment of stock position.

For efficient store-keeping, a separate Stores Department under the headship of a ‘store-keeper’ is set up. The store-keeper is a man of wide experience in stores routine. He is assisted by a number of store-men in the performance of his duties. The store-keeper is responsible for the safe performance of his duties. The main duties and responsibilities of a store-keeper are:

To issue requisition on purchase department for purchasing materials at the right time.
To accept into stores, materials supplied by suppliers or returned by production departments.
To check in all materials as to quality and quantity.
To keep all the materials in safe and convenient manner in appropriate bins and containers.
To issue materials against proper authorization.
To maintain proper records of receipts, issues and balance of materials.
To watch levels of stock and replenish materials when necessary.
To prevent the entry of unauthorized persons into the stores.
To advise the management on the day-to-day affairs of the stores department.
To dispose of scrap or obsolete materials.
Location Of Stores
‘Location’ means the site for the store. The location of the stores should be carefully planned. An important factor to be considered when establishing a store set up is the question of locating it in the most appropriate place. The stores must be set up at a convenient and safe place, near to Receiving Department, easily accessible from all parts of the factory and by means of transport and free from the risk of fire, theft, etc. The general principle in determining the location of stores is to minimize the total kg. — km. cost of transportation of materials.

Factors determining the location of stores
The main factors which determine the location of store in a manufacturing concern may be given as follows:

1. Minimization of Material Handling Efforts: Minimisation of material handling efforts implies location of raw material store near the production shops and location of finished goods store and packing materials store near the assembly shop. The stores should be easily accessible by means of transport.

2. Nature of the Materials: The nature of the materials to be stored also affects the location of the store. Material that is not damaged by weather can be stored out of doors in a shed. But materials such as cement, plaster, etc., must not only be protected from the weather but must also be stored in a dry place.

3. Quantity, Weight, etc., of the Materials: The quantity of each of the goods to be stored must be taken into account for determining the location. When the quantities are known, adequate provision may be made for immediate and future storage needs.

4. Flow of Materials: Location of store should be convenient which allows for steady and regular flow of store items without any obstruction.

5. Free from Risk of Loss: Store must be set up at a safe place which is free from the risk of loss due to fire, theft, moisture, etc.

6. Flexibility: The location of store must be such which provides for its future expansion.

Layout of stores
‘Layout’ of stores refers to the physical arrangement of storage facilities or the internal arrangement or placement of materials inside the stores. Layout of stores aims at effective utilization of space available for storage of materials, making the receipt and issue of stores convenient, giving a better appearance to the store and reducing the chances of damage, wastage, pilferage and accidents.

It also aims at reducing the operating cost of storage. The layout of stores should be determined according to the class and quantity of materials to be stored and the general nature of the business. There should be proper and separate arrangement for different items of materials from the viewpoint of the economy in space, effective supervision, minimum of wastage and convenience in issue. The materials should be kept in bins, racks, shelves, drawers, drums, packages and containers.

Factors to be considered for determining stores layout
1. Similarity: Items of similar nature should be stored at one place for the sake of easy identification and convenient issue.

2. Popularity: The turnover of each item of stores should be considered so that fast moving items should be stored near the point of issue/usage.

3. Size of Item: Items of store which are large or bulky in nature should be stored near the point of use.

4. Nature of Materials: Nature of materials to be stored is also important in determining the layout of store. Hazardous, sensitive and perishable goods should be stored separately at safe places.

5. Physical Movement of Materials: The principle of ‘first-in-first-out’ should be strictly adhered to in the matter of physical movement of the materials.

6. Physical Facilities: Efficient layout should also consider the various physical facilities such as lighting arrangement, ventilation, wall paints, size of platforms, availability of cranes and handling equipment.

MAELEZO KUTOKA KWA KATIBU MKUU UTUMISHI.

MAELEZO KUTOKA KWA KATIBU MKUU UTUMISHI.

1. Malimbikizo ya salary, yatalipwa automatic baada ya areas kuwa approved na maafisa utumishi, kuanzia pale ulipopanda. Hakuna tena kudai area

2. Uhamisho, kuhamisha mshahara ni jukumu la mwajiri wa awali, kama umehama

3. Kuhama mkoa ni lazima jina litokee kwenye orodha ya watumishi wanaohama.

4. Kwa wastaafu wanaodai areas, wanatakiwa kujaza fomu na viambatanishi ili ulipwe nje y

5.Malimbikizo ya mshahara kuonekana kisha kufutika, haijapotea ila inahitaji kuidhinishwa upya.

6.Kama hujapata areas, na madai ni ya muda mrefu fuatilia kwa afisa utumishi ili ujaze form maalum.

7. Ukipanda cheo, kiri haraka.

8.Posho za safari za kikazi zinatokana na status ya mtumishi, upandishaji wa vyeo vya watumishi hutegemea vikao vya DED, upandaji cheo inategemea fungu lililopangwa, mtumishi haruhusiwi kudai cheo. Hii ni kanuni. Promotion ni motisha kwa watumishi, si automatic. Mwajiri lzm apate taarifa za utendajikazi wa utumishi ndipo aandae promotion.

9.Madai kwa watumishi waliohama, yatashughulikiwa na mwajiri wa sasa baada ya kuwasiliana na mwajiri wa awali.

10. Upatikaji wa nyaraka www. Tanzania. Go. Tz, www. Utumishi. go. Tz na www. Tamisemi. Go. Tz, utapata nyaraka na huduma kwa kutumia simu au computer.

11. Nauli za likizo, inategemea bajeti ya halmashauri, ilipwe kabla ya kusafiri, akijisafirisha atadai. Maombi ya nauli za likizo yatahakikiwa kwa kutumia nauli za SUMATRA. Marufuku kulipwa nusu nauli.

12. Kusoma nje ya nchi, kama upo kwenye mpango wa mwajiri utalipiwa na kulipwa mshahara, kama haupo mwenye mpango, utachukua likizo bila malipo. Kibali kitatolewa na katibu mkuu kusafiri nje.

13. Rufaa ya matibabu, mwajiri alipe nauli na posho ya kujikimu. Ukijigharamia, mwajiri anatakiwa kukulipa.

14. Kutofautiana kwa mishahara kwa watumishi wenye sifa zinazofanana, kuna tume ya job evaluation inafanya utafiti hatua za mwisho, pia tatizo lilikuwa tsd kutoshirikiana na mkurugenzi. Lkn tsd imekuwa tsc, tatizo litakwisha.

15. Disturbance allowance italipwa kwa 10% ya mshahara wake wa mwaka. Kwa watumishi waliohama destination, hata kama ni ndani ya km5.

16. Tumekumbushwa kutunza nyaraka, kufuatilia mifuko ya jamii na michango ili kuhakiki uwasilishaji wa michango kabla ya kustaafu

17.Uteuzi wa wakuu wa idara huzingatia: utendaji kazi, uongozi, royality, elimu, nk.

18. Tange kwa kila kada ijazwe na kuwasilishwa kwa afisa utumishi.

19. Waliocheleweshwa kupanda daraja, wanatakiwa kwenda kwa afisa utumishi ili ajenge hoja ya kupanda kwa mseleleko na kuomba kibali kwa katibu mkuu.

20. Kama uliwekwa kwenye mpango wa mafunzo halafu ukajipia, mwajiri anatakiwa akurudishie gharama alizotakiwa kukulipia.

21. Punguzo la kodi ya mshahara 9% linahusu wenye mishahara ya chini. Yeye katibu mkuu anakatwa 30% ya mshahara.

22.May 2016 promotion zilisitishwa pamoja na mishahara ilisitishwa kwa ajili ya watumishi hewa. Vyeo vyao vipo, ila marekebisho yao yamesitishwa. Watarejeshwa ktk vyeo vyao vipya soon.

23. Uhakiki bado serikali kuu.

24.Vyeo vya kielimu ktk nchi kimuundo ni mpaka 1st degree. Masters, phd ni mbwembwe

25. Mishahara ya watumishi italingana na uzito wa kazi, miundo ya utumishi kurekebishwa ili watu wasifike bar/vidato vya mshahara.

26. Madeni yaliyokataliwa, yafuatiliwe ili kama ni tatizo la document, zitafutwe na kuprossess upya deni.

27. Walimu wa sayansi wanaofundisha na kufanya laboratory technicians wapewe allowances. Wataalam wa laboratory wanaandaliwa.

28. Kukaimu madaraka mwisho miezi 6, athibitishwe au asitishwe.

Siri za Ndege: Kesi ya Kudadisi ya Ndege ya Pan Am 914.

Kasomi Tv
Siri za Ndege: Kesi ya Kudadisi ya Ndege ya Pan Am 914.

Ndege ilisafiri kutoka New York City mnamo 1955 na ilitua Venezuela mnamo 1985, au ilikuwa 1992? 
pan-am-dc4-422x305.jpg


Siri

Pan Am Flight 914 ilikuwa Douglas DC-4 na abiria 57 na wafanyikazi sita ambao waliondoka kutoka uwanja wa ndege wa New York City kuelekea Miami, Florida. Tarehe ilikuwa Julai 2, 1955. Ndege hiyo ilipangwa kudumu masaa kadhaa, lakini haikuwasili Miami. Badala yake, ilionekana, bila kutangazwa na isiyoonekana kwa rada ya Caracas, mnamo Machi 9, 1985! Akielezea wasiwasi wake kwa mnara huo, rubani, baada ya kutua kwa kitabu, aliandika tax kuelekea lango, na washughulikiaji wa ardhi waliweza kuona sura za abiria wanaopiga kelele wakiwa wamebanwa juu ya windows zao, wakiangalia ulimwengu mpya mzuri. Kwa upande wake rubani, alitupa kalenda ndogo nje ya dirisha kabla hajarudi haraka kwenye barabara ya kurukia, ambapo alisimama na kutoweka ghafla kama alikuwa amefika. Na kalenda? Je! Aliiacha kwa bahati mbaya? Au inashikilia siri ya kile kilichotokea? Ilisema nini haswa?

Hatuwezi kujua kamwe. Serikali ya Venezuela na Merika, hadithi inasema, ilisemekana walichukua kalenda na kanda za mnara na wamekataa kutoa maoni juu ya tukio hilo hata mara moja katika miongo kadhaa iliyoingilia. Je! Ni nini kilitokea kwa Ndege 914?

Ni, kwa mara moja, siri ambayo ina jibu.

Nadharia

Hadithi imekuwa ikizunguka mtandao kwa miaka na ni mada moto ya jukwaa na UFO na umati wa kusafiri wakati.

Nadharia maarufu zaidi ni kwamba ndege ilipitia aina fulani ya bandari ya muda au minyoo, na badala ya kutua Miami mnamo 1955, ilionekana wakati wa kuwasili Venezuela miaka 30 baadaye. Mtu anafikiria ilirudi kupitia minyoo baada ya kuondoka Caracas. Hasa jinsi minyoo au milango ya wakati inavyofanya kazi haieleweki vizuri, inaonekana.

Ukweli

Kama unavyotarajia tayari, hadithi ya Pan Am Flight 914 ilikuwa uzushi wa jumla. Lakini katika kesi hii, tofauti na hadithi nyingi za mijini, chanzo cha uzushi huo kinajulikana.

Imeanzia kwenye hadithi iliyochapishwa kwanza mnamo 1985 na The Weekly World News, jarida la wakati mmoja (sasa wavuti), ambalo lina utaalam katika hadithi za wazimu, zilizoundwa kama hii. Jarida liliandika hadithi hiyo tena mara mbili katika miaka ya 1990 (na tarehe ya kuwasili kwa ndege ilibadilishwa kuwa 1992 katika hadithi hizo za baadaye).

Hadithi hiyo ilipata msukumo mkubwa wakati idhaa ya YouTube ya Bright Side ilipoweka video kuhusu kutoweka. Video iliyotengenezwa kwa urahisi imepata maoni zaidi ya milioni 15, lakini haifikii ukweli kwamba ilikuwa hadithi bandia ya bandia hadi karibu theluthi mbili kupitia. Bright Side ilianzisha "maelezo" kadhaa ambayo hayakuwa katika hadithi ya kwanza ya Wiki ya Dunia ya Wiki, pamoja na ukweli kwamba ndege hiyo ilionekana kwenye rada. Kwa hali yoyote, video inaonyesha kwamba hadithi hiyo ni uwongo tu hadi mwisho.

Inawezekana kwamba wengine walifaidika na habari hizi bandia za kweli kushiriki hadithi bila kuongeza kwamba maelezo muhimu, ile juu ya jinsi kila mtu alijua wakati wote wa jambo hilo lilikuwa la uwongo. Yote yanaenda kuonyesha jinsi watu wanavutiwa na ndege, hata wakati hadithi imeundwa ili kuunda hisia za kawaida.





Ijumaa, 16 Aprili 2021

Mikoa 10 yenye wasomi wengi Tabmnzania

 1.MKOA WA MARA huu umeshika nafasi ya kwanza ambao unapatikana kanda ya ziwa kwa kutoa wasomi wengi zaidi ambapo mkoa wa mara wanapatikana WAGITA,WAJALUO, WAKURYA NA WAZANAKI ambao kwa kiwango kikubwa ni jamii zilizoenda shule 


2.KILIMANJARO huu ni mkoa unashika nafasi ya pili ambapo mkoa unapatikana kaskazini huu umeshikiliwa na makabila mawili makuu WACHAGA NA WAPARE ambao ni wasomi wa kiwango cha juu zaidi na wengi wameenda shule 

3.MWANZA ni mkoa upo kanda ya ziwa ambao yanapatikana makabila matatu nayo wasukuma,wazinza na wakerewe ambapo hizi ni moja kati ya jamii zilizoenda shule sana ni jamii zilizotoa wasomi wengi zaidi 

4.KAGERA ni mkoa ambao upo kanda ya ziwa yanapatikana makabila manne ambayo ni wangaza,wasubi,watusi wanyambo na wahaya huu ni mmoja kati ya mkoa unashika nafasi ya nne kwa kutoa wasomi wengi zaidi .

5.MBEYA huu ni mkoa unaopatikana kanda za juu kusini ambapo yanapatikana makabila makuu mawili wasafa na wanyakyusa pia mkoa huu umetoa wasomi wengi zaidi licha wengi kuonekana wametokea unyakyusani

6.TABORA ni mkoa unaopatikana kanda ya kati ambapo wenyeji wa mkoa huu ni wanyamwezi, watusi, wasukuma pamoja na wamanyema 
pia mkoa huu unashika nafasi ya sita kwa kutoa wasomi wengi zaidi licha wengi kuonekana wanyamwezi

7.ARUSHA huu ni mkoa wanaopatikana wameru, waarusha, wamasai mkoa huu upo kanda ya kaskszini pia mkoa huu unasemekana kutoa wasomi wengi zaidi


8.RUVUMA ni mkoa ambao wenyeji wake ni wangoni,wamatego na wamatumbi huu ni mkoa ambao umetoa wasomi wengi zaidi wengi wao wakionekana kutokea jamii za kingoni

9.IRINGA huu ni mkoa ambapo upo nyanda za juu kusini ambao wenyeji wake wengi ni wahehe,wabena, wanyarukoro,wakinga huu ni mkoa ambao umetoa wasomi wengi zaidi wengi wakitokea jamii za wakinga na wabena

10.KIGOMA huu ni mkoa unaoshika nafasi ya kumi ambapo wenyeji wa mkoa huu ni waha,wamanyema, wabwaliii, wabangubangu, watusi pia kigoma ni miongoni ya mikoa iliyotoa wasomi wengi zaidi.

Endelea kua mwanafamilia wa EmmanuelKasomi

Historia ya Tundu A. Lissu

 

Historia ya Tundu A. Lissu

 


Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu alinusurika kushambuliwa na mbunge wa zamani wa Bunda, Steven Wasira katika moja ya vikao vya Bunge mjini Dodoma.

Lissu alisema hayo wakati akisimulia sehemu ya maisha yake binafsi na mambo aliyowahi kukutana nayo maishani katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika Jumatano.

Katika simulizi hiyo, Lissu, ambaye kwa sasa ni rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), alizungumzia pia kesi zinazomkabili, maisha ya mahabusu, familia, kazi zake, burudani anazopenda na mahusiano yake na watu wa aina tofauti.

Akizungumzia mkasa uliosababisha anusurike kupata kipigo hicho, Lissu alisema Wasira alikuwa amechukizwa na maneno yake makali bungeni.

“Nilikuwa nimemuudhi kwa kumtolea maneno makali wakati nikichangia,” alisema Lissu akijaribu kukumbuka alichosema.

Pamoja na kutokumbuka alichokisema, wakati huo Lissu alimponda Wasira kuwa alijiunga upinzani kwa kuwa alidhani kuna fedha na alipogundua hakuna ndipo akakimbia kurudi CCM.


“Alichukia sana. Sasa nimetoka pale naenda chooni, nikamkuta akiwa na wabunge wengine wa CCM. Aliponiona akaanza kunifuata akiniambia kuwa atanipiga,” alikumbuka Lissu.

“Akichukia anakuwa mkubwa kweli, na mimi mdogo. Anakuwa tofauti na niliona anaelekeza kwenye kona ili anipate vizuri. Nikiangalia kama wale wabunge wengine wa CCM wataingilia kuamulia, naona hakuna anayetaka kumzuia.

“Nilikuwa natamani mtu aje aingilie, nichomoke, lakini hawakujishughulisha nasi. Akarusha ngumi ya kwanza, nikakwepa. Akanisogelea tena, akarusha ngumi nyingine ikanikosa. Hapo sasa nikawa napiga hesabu. Nikasema akisogea tena, nampiga teke, na akiinama tu kuugulia, mimi nachomoka.”

Hata hivyo, Lissu alisema, Wasira hakuendelea na badala yake akageuka na kuanza kuondoka.

“Hapo ilikuwa pona yangu. Yule anatisha akichukia,” alisema.

Hata hivyo, Wasira amedai Lissu hasemi ukweli.

Lissu analichukulia tukio hilo kuwa la kawaida katika maisha yake ya mapambano ya kutetea mazingira, haki za wanyonge na kupigania demokrasia na utawala bora.

Akijibu swali kuhusu hali ya usalama wake katika maisha anayoendesha ya mapambano, Lissu alisema hajawahi kutishiwa maisha yake kwenye siasa na anakumbuka ni mara moja tu alitishiwa maisha wakati akipigania mazingira.

“Kuna watu wana hasira na mimi kwelikweli, lakini hawajawahi kunitishia,” alisema.

“Nakumbuka zamani kabla sijawa mbaya namna hii, twenty years ago, wakati nikiongoza Chama cha Wanasheria Watetezi wa Mazingira (LEAT) niliwahi kupata vitisho,” alisema Lissu.

Alisema wakati huo Serikali ya Awamu ya Tatu ilimpa raia wa Ireland, Reginald Nolan eneo kwenye delta ya Rufiji ili aendeshe mradi wa kuvuna kamba.

Alisema Serikali ilimpa hekta 20,000 ili atengeneze mabwawa ya kufuga kamba kwenye delta ya Rufiji, maeneo ambayo yana vijiji vinane, shughuli za kilimo na makazi na msitu ya mikoko.

“Niliongoza kampeni ya kimataifa kwa kila njia, ikiwamo mitandao ya kimataifa ya wanaharakati kuupinga mradi huo. Hatimaye, Benki ya Vitega Uchumi ya Ulaya (European Investment Bank) iliyokuwa itoe mkopo kwa Nolan ambao ungedhaminiwa na Serikali ya Tanzania, wakasema hawatatoa mkopo na kwa hiyo, mradi mzima ukasambaratika,” alisema.

“Wakati huo ndipo tukaletewa barua ya vitisho iliyopitishwa chini ya mlango. Asubuhi ndipo tukaikuta. Lakini zaidi ya hapo sijawahi kupata vitisho.

“Kwanza watanitishia nini? Wataniambia nyamaza tutakuua?”

Hata hivyo alisema anajua hayuko salama kutokana na aina ya siasa anazoendesha.

“Huwezi ukawa unaendesha siasa za aina hii halafu ukawa salama. Lazima utegemee kusumbuliwa. Usipotegemea kusumbuliwa, utapata shock,” alisema.

Lissu alisema hata matukio ya kukamatwakamatwa na askari wa Jeshi la Polisi hayajawahi kumshangaza kwa kuwa amekuwa akiendesha siasa za mapambano.

“Na wala sikosi usingizi. Nilale central (kituo kikuu cha poli) au nilale nyumbani, napata usingizi wangu mzuri kabisa,” alisema Lissu.

“Ili mradi nipate chupa zangu tatu kubwa za maji ya Kilimanjaro. Hizi chupa huwa nazitumia kama mto. Nikizipata tu, naweka kichwani na nalala usingizi mzuri kabisa. Tena mimi huwa nakoroma. Ndio maana nikitoka mahabusu huwa mnaniona nimebeba chupa ya maji ya Kilimanjaro.”

Hata hivyo, Lissu alisema hafurahii maisha ya mahabusu kwa kuwa si sehemu nzuri.

“Kusema sikosi usingizi, hakumaanishi kuwa nafurahia kulala mahabusu, hasa unapokuwa huna kosa,” alisema.

“Huko kuna watu wengi wanakamatwa na kuwekwa mahabusu bila ya makosa. Si kitu kizuri.”

Alisema hadi sasa ameshakaa mahabusu kwa kesi nne, ambazo zote ni za uchochezi. Akizungumzia jinsi anavyoweza kumudu maisha ya kifamilia, uwakili, ubunge, uongozi wa Chadema na urais wa TLS, Lissu alisema hayo yote yanawezekana kama unajipanga.

“I’m a very busy man (ni mtu niliye na kazi nyingi), lakini nimejifunza kitu. Fikiria tunatumia muda kiasi gani kwenye kinywaji. Kwa hiyo there’s plenty of time (kuna muda mwingi),” alisema Lissu.

“Napata muda wa TLS, tuna vikao viwili, muda wa kukaa na mama, wa Chadema, na napata muda wa mahakamani, Napata muda wa kinywaji. Mimi nakunywa Tusker ya baridi.

“Ukipanga muda wako sawasawa, there’s plenty of time.”

Lakini alisema kutokana na harakati ambazo zimekuwa zinamkabili, mwaka jana hakupata muda wa kutosha wa kuwa karibu na wapigakura wake wa Jimbo la Singida Mashariki.

“Najua hilo lina gharama zake, lakini ni lazima nifanye kazi zote,” alisema.

Lissu alisema kati ya mambo hayo, hupata muda wa kutosha wa kusoma kwa kuwa hicho ndicho kitu anachokipenda sana maishani mwake.

“Nikisafiri, iwe kwa ndege au kwa gari, ni lazima niwe na vitabu, magazeti. Hata nikiwa gerezani huwa naenda na magazeti,” alisema Lissu.

“Kwa kweli, ikitokea kwamba ninahukumiwa kufungwa, kitu ambacho kitanisumbua sana ni kukosa freedom ya kusoma.”

Lissu amekuwa akihusika katika kesi lukuki, kuanzia zile za kawaida za ofisi yake, za kisiasa zinazohusu wanachama wa Chadema, za wananchi na zinazomkabili, lakini anasema mashauri hayo hayajamfanya awe tajiri.

“Mimi si tajiri, ni mtu wa kawaida. Kazi yangu kubwa ni kutoa msaada wa kisheria,” alisema.

“Nimeoa Tarime, mke wangu ni mwanasheria na anatoka Tarime. Huko mimi ni maarufu sana, lakini si kwa sababu ya mke wangu.

“Huko nilitoa watu 466 gerezani ambao walikuwa wamefungwa kutokana na kupinga kunyang’anywa ardhi.”

Alisema hiyo ilikuwa wakati wawekezaji walipokuwa wakipewa ardhi kwa ajili ya kuchimba madini.

Alisema wateja wake wengine wakubwa kwa sasa ni vijana wanaoshtakiwa kwa makosa ya mtandaoni.

“Sheria mbili za makosa ya mtandaoni zimesababisha watu wengi kukamatwa. Wote wamekuwa wateja wangu,” alisema.

“Usipowatetea hawa wadogo wasio na kitu na wasioweza kusema, siku mkianza kushughulikiwa hakuna atakayewatetea.”

Alisema shughuli hizo huzifanya kwa kutoa msaada na anamudu kufanya hivyo kwa kuwa ni mbunge.

“Mshahara wa ubunge unaniwezesha kutetea Watanzania mahakamani. Fedha kidogo ninayopata ndiyo ninayoitumia kusafiri na gharama nyingine. Si tajiri, lakini naishi confortably,” alisema.

Alisema tofauti na mawakili wengine, kazi yake haina gharama kubwa za uendeshaji kwa kuwa ameziepuka.

“Kwanza ofisi yangu iko nyumbani. Pale ndipo nafanya kila kitu, kwa hiyo hakuna cha kumlipa msichana wa usafi,” alisema mbunge huyo wa Singida Mashariki.

Kuhusu mjadala uliotuama mitandaoni ikimtaja Nape Nnauye kuwa shujaa baada ya kupinga uvamizi wa kituo cha televisheni cha Clouds Media uliofanywa na kiongozi wa Serikali aliyeambatana na askari wenye silaha za moto, Lissu alisema mbunge huyo wa Mtama si shujaa na kumfananisha na waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Ghana, Tawia Adamafyo.

“Huyu mtu amezima Bunge na kulivuruga kwelikweli. Amefungia magazeti. Akiwa waziri amepitisha sheria ya mbovu ya Huduma ya Vyombo vya Habari, sioni ushujaa wowote bali amevuna matunda ya kazi yake na siasa za ndani ya CCM,”alifafanua

Tawia aliwasilisha muswada wa kuwaweka ndani watu enzi za Kwame Nkrumah, sheria ambayo ilipigiwa kelele na wabunge.

“Huyo Tawio hakujua sheria anayotunga inatengeneza rat trap (mtego). Kilichotokea ni yeye kuwa wa kwanza kuwekwa kizuizini kwa kutumia sheria hiyo maofisa usalama kutegesha bomu karibu na eneo alilokuwa akihutbia Rais Nkurumah na hivyo waziri huyo kuonekana alihusika.

“Hawa viongozi wanatunga sheria wanazodhani zitawabana na kuwashughulikia wapinzani, yakiwakuta wao wanapiga kelele. Kwahiyo mimi sioni ushujaa wowote wa Nape,”alieleza Lissu ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa Chadema.

Nape alivuliwa uwaziri wa habari Machi 23 baada ya kuachwa kwenye mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.
Na Emmanuel kasomi

Historia ya Grand P

Grand P Msanii Mwenye Mvuto wa Aina Yake  Thread starte Jina la kuzaliwa:   Moussa Sanguiana Kaba  Mwaka wa kuzaliwa: 1990 Umri: Miaka 31(mw...